TANZANIA YASISITIZA UMUHIMU WA TAKWIMU KIUCHUMI.
Serikali ya Tanzania imeushauri Umoja wa Mataifa kuanzisha mfumo thabiti wa takwimu utakaosaidia kupata taarifa sahihi kuhusu masuala ya uchumi kuelekea azimio la Ajenda ya Hatua ya Addis Ababa.
Wito huo umetolewa na Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, Bi. Amina Khamis Shaaban, mjini Addis Ababa nchini Ethiopia, kwa niaba ya Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), wakati wa kufunga kikao cha kwanza cha Kamati ya Maandalizi ya Mkutano wa Nne wa Kimataifa wa Ugharamiaji kwa Maendeleo Endelevu (Fouth International Conference on Financing for Deveoplopment - FfD4 unaotarajiwa kufanyika mwakani.