TANZANIA YASISITIZA UFADHILI ENDELEVU WA AFYA KUPITIA RASILIMALI ZA NDANI.

Waziri wa Fedha wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Balozi Khamis Omar (Mb), akishiriki kama mwanajopo katika mjadala wa Mawaziri wa Fedha na Afya, kuhusu "Ufadhili Endelevu wa Afya: Kugharamia Mustakabali wa Afya Barani Afrika katika Kipindi cha Ufinyu wa Bajeti na Kujitegemea katika Masuala ya Afya." kabla ya Kikao cha Sabini na Sita cha Kamati ya Kanda ya Shirika la Afya Duniani (WHO) kwa Kanda ya Afrika, Jijini Addis Ababa nchini Ethiopia.