TANZANIA YASHIRIKI MKUTANO WA 6 WA WATAALAMU WA NCHI WANACHAMA WA AU
Naibu Katibu Mkuu - Wizara ya Fedha, Bi. Amina Khamis Shaaban, ameongoza ushiriki wa Tanzania katika Mkutano wa 6 wa Wataalamu wa masuala ya Fedha, Mipango ya Kiuchumi na Ushirikiano, kwa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika. Kikao hicho kinafanyika tarehe 17 hadi 19 Julai 2023, katika ukumbi wa hoteli ya Movenpick, jijini Nairobi, nchini Kenya.