TANZANIA YASHIKA UKURUGENZI WA BENKI YA MAENDELEO YA AFRIKA

Tanzania inatarajia kushika nafasi ya Mkurugenzi Mtendaji mbadala (Alternative Executive Director) katika Kundi la Magavana wa Afrika Mashariki katika Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) kuanzia mwezi Agosti, 2024. Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-Maamry Mwamba ameyasema hayo kwa niaba ya Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), wakati wa Mkutano wa kawaida wa Magavana wa Kundi la Nchi za Afrika Mashariki ambao ni wanachama wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) ikiwa ni maandalizi ya Mikutano ya Mwaka 2024 ya Bodi ya Magavana (Mawaziri wa Fedha kutoka nchi wanachama) wa Benki hiyo inayofanyika Jijini Nairobi nchini Kenya.