TANZANIA YASAINI MKATABAWA BILIONI 988 KUENDELEZA MIUNDOMBINU JIJINI DAR ES SALAAM

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb) (kulia), na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia nchini Tanzania, Bw. Nathan Belete, wakibadilishana hati ya mkataba wenye thamani ya Euro milioni 361.1 (sawa na takribani shilingi bilioni 988.093) kwa ajili ya kutekeleza Awamu ya Pili ya Mradi wa Kuendeleza Miundombinu Dar es Salaam (Dar Es Salaam Metropolitan Development Project Phase II (DMDP II). Hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Hazina Ndogo, jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa pia na Waziri wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Mohamed Mchengerwa (Mb), Naibu Waziri wa TAMISEMI, Mhe. Deogratius Ndejembi, Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Mhe. Khamis Hamza Khamis, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, Wabunge wa Mkoa wa Dar es Salaam wakiongozwa na Mwenyekiti wao Dkt. Faustine Ndugulile, Viongozi waandamizi wa Serikali pamoja na Viongozi wa Mkoa wa Dar es Salaam.