TANZANIA YAPOKEA MKOPO WA SH. BILIONI 32 KUTOKA SAUDI ARABIA

Tanzania imepokea mkopo wa dola milioni 13 sawa na shilingi bilioni 32 kutoka Mfuko wa Maendeleo wa Saudi kwa ajili ya ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme kutoka Benaco hadi Kyaka mkoani Kagera. Mkataba wa mkopo huo umesaiiniwa na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba kwa niaba ya Serikali ya Tanzania na Mkurugenzi Mtendaji wa mfuko huo Bw. Sultan Almsarshad, wakati wa Mkutano wa Masuala ya Uchumi kati ya Nchi za Kiarabu na Afrika uliofanyika Riyadh- Saudi Arabia.