TANZANIA YAISHAURI BENKI YA DUNIA KUWEKA VIPAUMBELE KATIKA MIRADI YA MAENDELEO AFRIKA
TANZANIA imeishauri Benki ya Dunia kutilia maanani vipaumbele vya maendeleo vya nchi za Afrika ikiwemo kuzipatia fedha na ujuzi ili ziweze kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.
Rai hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba kwa niaba ya Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (MB), kwenye Mkutano wa Mawaziri wa Fedha na Magavana wa Kundi la Kwanza la Nchi za Afrika la Benki ya Dunia) (WBG Africa Group 1 Constituency) uliofanyika Washington DC, nchini Marekani.