TANZANIA YAENDELEA KUJIDHATITI KATIKA UZUAJI WA UTAKASISHAJI WA FEDHA HARAMU

Tanzania imekuwa mojawapo ya nchi zilizo Mashariki na Kusini mwa Afrika zilizopiga hatua kubwa katika udhibiti wa utakasishaji fedha haramu na uzuiaji wa silaha za maangamizi na ufadhili wa ugaidi nchini. Naibu Waziri wa Fedha Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb), amesema hayo katika Mkutano wa 23 wa Baraza la Mawaziri na Maafisa Waandamizi wa Umoja wa nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika wa Kudhibiti Utakasishaji Fedha Haramu (Eastern and Southern Africa Anti Money Laundering Group (ESAAMLG), unaofanyika katika mji wa Kasane, nchini Botswana.