TANZANIA, USWISI NA IRELAND ZASAINI MKATABA WA KUNUSURU KAYA MASIKINI

Serikali ya Tanzania imesaini mikataba miwili ya msaada yenye thamani ya dola za Marekani milioni 20.3 sawa na shilingi bilioni 50.13 kwa ajili ya kunusuru kaya masikini awamu ya pili (PSSN II). Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba alisema msaada huo umetolewa na Serikali ya Uswisi dola za Marekani milioni 18 na Euro milioni 2.2 sawa na dola za Marekani milioni 2.3 zimetolewa na Serikali ya Ireland.