TANZANIA, QATAR ZATIA SAINI MKATABA WA KUONDOA UTOZAJI KODI MARA MBILI.

TANZANIA na Qatar, leo tarehe 29 Septemba, 2026, zimetia saini Mkataba wa Kuepusha utozaji kodi mara mbili na kuzuia ukwepaji kodi (Double Taxation Agreement). Waziri wa Fedha wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb) na Waziri wa Fedha wa Qatar, Mhe: Ali Bin Ahmed Al Kuwari, wamesaini Mkataba huo kando ya Mkutano wa 11 wa Mwaka wa Bodi ya Magavana wa Benki ya Maendeleo ya Miundombinu ya Asia (AIIB) uliofanyika jijini Doha nchini Qatar. Mhe. Balozi Omar amesema kuwa hatua hiyo imelenga kuboresha mazingira ya biashara kati ya mataifa hayo mawili, hatua itakayo kuza zaidi uchumi wa pande zote mbili.