TANZANIA NA UN ZASAINI MPANGO KAZI WA PAMOJA

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Umoja wa Mataifa (UN) wamesaini Mpango Kazi wa pamoja wa Mwaka 2023/24 wa ushirikiano wa maendeleo kati ya Serikali na Mashirika ya Umoja wa Mataifa. Hati za Mpango kazi huo zimesainiwa jijini Dodoma na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba na Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa na Mwenyekiti wa Kundi la Washirika wa Maendeleo nchini, Bw. Zlatan Milišić, katika Kikao cha Pili cha Kamati ya Usimamizi wa Mpango wa Ushirikiano kati ya Tanzania na Mashirika ya Umoja wa Mataifa.