TANZANIA NA UAE ZATIA SAINI MKATABA WA KUTOTOZA KODI MARA MBILIKUBALI KATI YA NCHI HIZO

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Umoja wa Falme za Kiarabu zimetia saini mkataba wa makubaliano ya kuondoa utozaji Kodi Mara Mbili na Kuzuia Ukwepaji wa Kodi ya Mapato kati ya nchi hizo mbili, yaani Agreement on Avoidance of Double Taxation and Prevention of Fiscal Evasion on Income Taxes.