TANZANIA NA OMAN KUSHIRIKIANA KATIKA MAENEO MUHIMU YA MAENDELEO.

Tanzania na Oman zimekubaliana kuendeleza ushirikiano katika nyanja mbalimbali za maendeleo ikiwemo Sekta ya Nishati na Madini, kutengeneza mazingira bora ya uwekezaji, kubadilishana uzoefu na mafunzo katika masuala ya kodi pamoja na kuondoa utozaji kodi mara mbili kwa wawekezaji na wafanyabiashara watakaofanya shughuli zao kati ya nchi hizo mbili. Hayo yamesemwa wakati wa kikao cha Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Oman nchini Tanzania, Mhe. Saud Al-Shidhani, katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha Jijini Dar es Salaam.