TANZANIA NA JAPAN ZAISAINI MKATABA WA MSAADA WA BILIONI 27.3 KUSAIDIA SEKTA YA AFYA

Tanzania na Japan kupitia Shirika lake la Maendeleo (JICA), zimetiliana saini mkataba wa msaada wa Yen za Japan bilioni 1.527 (sawa na shilingi bilioni 27.3) kwa ajili ya kuboresha sekta ya afya nchini. Mkataba huo umesainiwa katika Ofisi za Hazina Ndogo jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, kwa niaba ya Serikali ya Tanzania, Balozi wa Japan nchini Tanzania, Mhe. Yoichi Mikami na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Japan (JICA), Bw. Hitoshi Ara, kwa niaba ya Serikali ya Japan.