TANZANIA NA JAPAN KUIMARISHA USHIRIKIANO
Serikali imesema kuwa itaendela kushirikiana na Japan huku ikitoa wito kwa kampuni za Japan kuja kuwekeza nchini katika maeneo mbalimbali katika sekta zenye maslahi ya nchi zote mbili ikiwa ni pamoja na kukuza uwekezaji binafsi.
Wito huo umetolewa leo jijini Dodoma wakati wa Mkutano kati ya Naibu Katibu Mkuu Bi. Jenifa Christian omolo kwa niaba ya Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) alipokutana na kuzungumza na Bw. Naoki Yanase, Mkurugenzi Mkuu Kanda ya Afrika wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA).