TANZANIA NA IFC ZAJADILI USHIRIKIANO WA SEKTA YA UMMA NA SEKTA BINAFSI KWA MAENDELEO YA NCHI

Serikali ya Tanzania imerejea tena dhamira yake ya kushirikiana kwa karibu na Shirika la Fedha la Kimataifa (IFC) ili kuongeza uwekezaji wa sekta binafsi, kupanua miundombinu na kuharakisha Mpango wa Taifa wa mabadiliko ya nishati chini ya Dira ya Taifa ya Maendeleo (DIRA 2050). Akizungumza katika kikao na Mkurugenzi wa IFC Kanda ya Afrika Mashariki, Bi. Mary Porter Peschka, Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), alisifu mchango wa muda mrefu wa IFC katika kukuza sekta binafsi nchini Tanzania, akisisitiza kuwa ushirikiano huo utaendelea kuwa muhimu katika kufanikisha malengo ya muda mrefu ya maendeleo ya taifa.