TANZANIA NA BURUNDI ZAJADILIANA UJENZI WA SGR.

WAZIRI wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Miundombinu wa Burundi Mhe. Dieudonné Dukundane, kuhusu maendeleo ya Mradi wa Reli ya Kisasa SGR utakaoziunganisha nchi hizo mbili. Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika Dodoma, Viongozi hao wamesema kuwa mradi huo utakapokamilika utachochea biashara ya madini na kilimo pamoja na kuimarisha mahusiano ya kikanda na kukuza uchumi wa nchi hizo mbili.