TANZANIA NA BENKI YA DUNIA YASAINI MKATABA WA MIKOPO NAFUU NA MISAADA YA SHILINGI TRILIONI 1.3

Tanzania na Benki ya Dunia zimetiliana Saini mikataba miwili ya mkopo nafuu na msaada yenye thamani ya dola za Marekani milioni 579.93, sawa na shilingi trilioni 1.332.8, kwa ajili ya kutekeleza miradi miwili ukiwemo mradi wa maji safi na usafi wa mazingira pamoja na mradi wa kuboresha afya ya mama na mtoto. Waliotia Saini mikataba hiyo Jijini Dar es Salaam, ni Waziri wa Fedha na Mpango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia, Bw. Nathan Belete.