TANZANIA NA ABU DHABI ZATIA SAINI MKATABA WA KUJENGA NJIA YA KUSAFIRISHA UMEME BENAKO HADI KYAKA MKOA KAGERA

Tanzania na Mfuko wa Maendeleo wa Abu Dhabi wa Umoja wa Falme za Kiarabu zimetiliana Saini mkataba wa mkopo nafuu wa dola za Marekani milioni 30 sawa na shilingi bilioni 70 za Tanzania kwa ajili ya Ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme Msongo wa kV 220 kutoka Benaco hadi Kyaka na Upanuzi wa Kituo cha Kupoza Umeme cha Kyaka mkoani Kagera. Mkataba huo umetiwa saini Makao Makuu ya Mfuko huo Mjini Abu Dhabi na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba, kwa niaba ya Serikali, na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Maendeleo wa Abu Dhabi (Abu Dhabi Fund for Development), Mhe. Mohammed Saif Al Suwaidi.