TANZANIA KUTUMIA MFUMO MPYA WA USIMAMIZI WA MADENI (CS-MERIDIAN)

Serikali imeungana na nchi nyingine za Jumuiya ya Madola kwa kuanza kutumia Mfumo mpya wa Usimamizi wa Madeni (CS-Meridian) ambao utaboresha upatikanaji wa taarifa za madeni. Akizungumza jijini Dodoma wakati wa uzinduzi wa mfumo huo, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Jenifa Omolo amesema mfumo huo utaleta tija katika kuhifadhi taarifa za madeni pamoja na kuongeza uwazi wa takwimu za madeni hayo.