TANZANIA KUTUMIA FURSA ZA UWEKEZAJI KUTOKA BENKI YA AFREXIM

Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba amemuahidi Rais wa Benki ya Afrexim kuongeza mtaji wa ziada katika Benki hiyo ambayo Tanzania inamiliki hisa ili iwe na wigo mpana wa kuendelea kupata rasilimali fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo. Dkt. Nchemba ametoa ahadi hiyo jijini Dodoma alipokutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Benki ya Afrexim, Prof. Benedict Oramah, ambapo walijadili masuala kadhaa likiwemo fursa zinazotolewa na Benki hiyo.