TANZANIA KUNUFAIKA NA MKUTANO WA BENKI YA DUNIA UTAKAOFANYIKA ZANZIBAR

Tanzania inatarajia kunufaika na Mkutano wa Kimataifa wa Tathimini ya Muda wa Kati wa Mzunguko wa 20 wa Benki ya Dunia (IDA20 Mid Term Review) utakaofanyika Zanzibar kuanzia tarehe 6 hadi 8 Desemba, 2023, ukiwashirikisha wajumbe zaidi ya 3,000 kutoka mataifa takribani 100 duniani. Hayo yamebainishwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango-Zanzibar, Mheshimiwa Dkt. Saada Mkuya Salum, wakati akifungua kikao cha Kamati ya Maandalizi ya Mkutano huo, kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano Wa Wizara ya Fedha na Mipango, Unguja-Zanzibar.