TANZANIA KUIMARISHA ZAIDI MFUMO IMARA WA UFUATILIAJI NA UDHIBITI UTAKASISHAJI FEDHA HARAMU
Tanzania imeihakikishia Jumuiya ya Kimataifa inayojihusisha na ufuatiliaji na udhibiti wa Utakasishaji fedha haramu, ufadhili wa ugaidi na ufadhili wa silaha za maangamizi. Kwamba Serikali itaendelea kuimarisha na kuboresha mifumo yake ya udhibiti wa vitendo hivyo nchini.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Mhandisi. Mshamu Ali Munde (Mb), kwa niaba ya Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi. Khamis Mussa Omar (Mb), wakati wa Mkutano wa Kimataifa wa Ubadilishaji wa Taarifa za Udhibiti wa Fedha Haramu Duniani (EGMONT Group meeting), uliofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC), jijini Arusha.
