TANZANIA KUIMARISHA USHIRIKIANO NA JAPAN, IFAD.

Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), amekutana na kufanya mazungumzo kwa nyakati tofauti na Balozi wa Japan nchini Tanzania, Mhe. Yoichi Mikami na Mkurugenzi Mkazi wa Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD), Bw. Sakphouseth Meng, ambapo wamejadili namna ya kuimarisha zaidi ushirikiano kupitia utekelezaji wa miradi ya kimkakati ikiwemo nishati na kilimo. Akiwa na Balozi wa Japan, Mhe. Balozi Omar aliishukuru nchi hiyo kwa kuendelea kushirikiana na Tanzania katika nyanja mbalimbali za kiuchumi na kijamii kwa kusaidia utaalam, mikopo nafuu na misaada ya kiufundi ambayo imeisadia Tanzania kupiga hatua kupitia sekta za kilimo, elimu, na viwanda.