TAKWIMU SAHIHI MSINGI WA MAENDELEO NA UWEKEZAJI ENDELEVU – MUNDE

Serikali imetoa wito wa matumizi ya takwimu sahihi katika kuelekeza uwekezaji wa sekta ya maji, kilimo na miundombinu ili kuongeza uzalishaji, kukuza uchumi na kuboresha maisha ya wananchi. Wito huo umetolewa jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb) kwa niaba ya Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb) katika hafla ya maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika.