TAFITI ZENYE TIJA ZITATATUA CHANGAMOTO ZA KIUCHUMI

Wajumbe wa Kamati za Utafiti na Ubunifu, Kamati Elekezi, na Kamati ya Kiufundi wametakiwa kutekeleza majukumu yao kwa weledi, uwazi na ubunifu ili kuhakikisha kuwa tafiti zinazofanyika zinatoa mapendekezo yanayotekelezeka. Agizo hilo limetolewa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Bi. Jenifa Christian Omolo, wakati akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-Maamry Mwamba, katika uzinduzi rasmi wa Kamati za Utafiti na Ubunifu, Kamati Elekezi, na Kamati ya Kiufundi uliofanyika katika Ukumbi wa Kambarage, Treasury Square, jijini Dodoma.