TAASISI ZITUMIE FURSA ZILIZOPO KUONGEZA MAKUSANYO YA MAPATO YASIYO YA KODI
SERIKALI imezitaka Wizara, Taasisi na Mashirika ya Umma yanazokusanya mapato yasiyo ya kodi kutumia kikamilifu fursa zilizopo ili kuongeza mapato ya ndani na kuimarisha uwezo wa Serikali kugharamia huduma za wananchi na miradi ya maendeleo.
Wito huo umetolewa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Bw. Nsubili Joshua, kwa niaba ya Katibu Mkuu, Dkt. Natu El-Maamry Mwamba, katika kikao cha Maafisa Masuuli wanaohusika na ukusanyaji wa mapato yasiyo ya kodi kilichofanyika katika Ofisi za Hazina (Treasury Square), jijini Dodoma.
