TAASISI ZA WIZARA YA FEDHA ZAHIMIZWA KUWASILIANA KIMKAKATI

Wakuu wa Vitengo vya Mawasiliano wa Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Fedha na Mipango wametakiwa kuwasiliana kimkakati ili kufikisha taarifa zinazohusiana na Wizara pamoja na Taasisi zake kwa wananchi kwa kuzingatia viwango na kwa wakati. Rai hiyo imetolewa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Jenifa Omolo, ambaye aliwakilishwa na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Utawala na Rasilimali Watu (sehemu ya rasilimali watu), Bw. Benjamini Chilumba, katika ufunguzi wa kongamano la Wakuu wa Vitengo vya Mawasiliano wa Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Fedha na Mipango, lililofanyika mkoani Morogoro.