TAASISI ZA UMMA ZATAKIWA KUTUMIA MFUMO WA TANePS

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Hamad Hassan Chande, ameziagiza taasisi zote za umma zilizosajiliwa katika Mfumo wa kielektroniki wa Ununuzi wa Umma (TANePS) kuutumia mfumo huo kwa kuzingatia sheria na miongozo mbalimbali ili kutoiingiza Taifa katika hasara.