TAASISI YA MSAADA WA KISHERIA AFRIKA (ALSF) KUWAJENGEA UWEZO WANASHERIA NCHINI

Serikali ya Tanzania imeishukuru Taasisi ya Msaada wa Kisheria Afrika (ALSF) chini ya Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) kwa kuwajengea uwezo wataalam wa sheria katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Hayo yameelezwa na Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, Bi. Amina Khamisi Shaabani kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, baada ya kikao kati ya Tanzania na Taasisi ya Msaada wa Kisheria Afrika (ALSF) kilichofanyika kando ya Mikutano ya Mwaka 2024 ya Bodi ya Magavana (Mawaziri wa Fedha kutoka nchi wanachama) wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Jijini Nairobi nchini Kenya.