SHERIA MPYA YA UBIA MBIONI KUKAMILIKA

SERIKALI ipo katika hatua za mwisho za marekebisho ya Sheria ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP) ambapo hatua hizo zitawezesha utekelezaji wa miradi kuwa mzuri zaidi ikilinganishwa na huko nyuma. Hayo yamesemwa na Kamishna wa Idara ya PPP Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. David Kafulila, wakati akiwasilisha mada kuhusu Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP) kwenye semina elekezi kwa baadhi ya wahariri wa vyombo vya habari nchini, iliyolenga kuwajengea uelewa wa masuala mbalimbali yanayotekelezwa na Wizara, iliyofanyika ukumbi wa Hazina ndogo, jijini Arusha.