SERIKALI YAZIFUNDA TAASISI ZAKE KUHUSU MIRADI YA UBIA
Mkuu wa Kitengo cha Uchambuzi wa Miradi Kituo cha Ubia kati ya Sekta Binafsi na Sekta ya umma (PPP Center), Bw. Alfred Misana, akieleza namna ya kuandaa miradi kwa njia ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP), kwa washiriki wa mafunzo yaliyoandaliwa na Wizara ya Fedha kwa Taasisi za Serikali yaliyolenga kuwapa elimu ya matakwa ya Sheria ya Mikopo, Dhamana na Misaada, Sura 134 na Miongozo mbalimbali kwenye ufadhili wa miradi ya maendeleo, iliyofanyika katika ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania, jijini Dar es Salaam.