SERIKALI YAWASILISHA BUNGENI MAPENDEKEZO YA UKOMO WA BAJETI 2023/2024
Serikali imewasilisha bungeni Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa na Ukomo wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/24, ambapo imepanga kukusanya na kutumia jumla ya shilingi trililion 44.3.
Bajeti hiyo inajumuisha shilingi trilioni 29.2 kwa ajili ya matumizi ya kawaida na shilingi trilioni 15.1 kwa ajili ya matumizi ya maendeleo.