SERIKALI YAWASIHI WANANCHI KUTUMIA ELIMU YA FEDHA ILI KUKUZA UCHUMI

Wakazi wa Jiji la Mbeya wametakiwa kutumia elimu waliyoipata katika Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Kitaifa kubadilisha maisha yao hususan katika masuala ya usimamizi wa fedha. Rai hiyo imetolewa na Kamishna wa Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha, Dkt. Charles Mwamwaja, wakati akifunga maadhimisho hayo Jijini Mbeya.