SERIKALI YAWAASA WANAHABARI KUIBUA FURSA ZA SERA YA MNYORORO WA UGAVI.

Serikali imewataka wanahabari kutumia kalamu zao na weledi wao kuongeza uelewa wa umma kuhusu Sera ya Taifa ya Usimamizi wa Mnyororo wa Ugavi, 2025, kwa kuzingatia takwimu sahihi, kueleza fursa zinazotokana na Sera hiyo, pamoja na namna inavyolenga kuimarisha matumizi bora ya rasilimali za umma. Wito huo umetolewa na Mhe. Naibu Waziri wa Fedha, Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb), wakati akifungua mafunzo ya Siku mbili ya Wahariri wa Vyombo vya Habari na Wamiliki wa Mitandao ya kijamii ya Habari, katika ukumbi wa Hoteli ya Timeless, mjini Morogoro.