SERIKALI YAUNDA KAMATI KUTATUA MGOGORO WA ARDHI WILAYA YA IRAMBA MKOANI SINGIDA
SERIKALI imeunda kamati ya kutanzua mgogoro wa mipaka ya ardhi baina ya wananchi na Msitu wa Hifadhi ya Bonde la Wembere unaosimamiwa na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Wilayani Iramba mkoani Singida, uliodumu kwa muda wa miaka mitatu.
Hatua hiyo imechukuliwa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mheshimiwa Mary Masanja, alipotembelea eneo hilo lenye mgogoro, akiambatana na Waziri wa Fedha na Mipango, Mheshimiwa Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Iramba Magharibi.