SERIKALI YATHAMINI MCHANGO WA BENKI YA DUNIA KATIKA KUKUZA UCHUMI.

Serikali ya Tanzania imeeleza kuthamini mchango mkubwa wa Benki ya Dunia katika kuendeleza agenda ya maendeleo ya kijamii na kiuchumi nchini huku ikisisitiza dhamira yake ya kuendelea kuimarisha ushirikiano huo kwa manufaa ya wananchi. Hayo yameelezwa katika Hoteli ya Hyatt jijini Dar es Salaam na Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb) wakati wa hafla ya kumuaga aliyekuwa Mkurugenzi wa Benki ya Dunia katika nchi za Tanzania, Malawi, Zambia na Zimbambwe, Bw. Nathan Belete na kumkaribisha rasmi Bw. Firas Raad, aliyeteuliwa kushika nafasi hiyo ambapo Waziri Mkuu, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba alikuwa mgeni rasmi.