SERIKALI YASHAURIWA KUANZISHA KLABU ZA MASUALA YA FEDHA SHULENI

Serikali imeshauriwa kuwasimamia Wakuu wa Shule kuongeza kasi ya kuanzisha Klabu za mambo mbalimbali yakiwemo masuala ya fedha katika shule zilizopo nchini ili zitumike kutoa elimu hiyo pamoja na mambo ya kijamii. Ushauri huo umetolewa na Mlezi wa Klabu katika Shule ya Sekondari ya Kutwa Liwale, Mwalimu Mustafa Ahmadi Likambako, alipokutana na Timu ya Wataalamu kutoka Wizara ya Fedha ambayo ipo mkoani Lindi kutoa elimu ya masuala ya fedha kwa makundi mbalimbali ya wananchi wakiwepo wanafunzi, wafanyabiashara, wakufunzi na wajasiriamali.