SERIKALI YASAINI MKATABA WA DOLA ZA MAREKANI BI.1.28 ZA UJENZI WA SGR MAKUTUPORA HADI ISAKA

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imesaini mkataba wa kukamilisha mpango wa ufadhili wa pamoja wenye thamani ya takribani dola za Marekani bilioni 1.277 kwa ajili ya kuendeleza mtandao wa Reli ya Kisasa (Standard Gauge -SGR), kipande cha tatu (loti 3) na cha nne (loti 4) kutoka Makutupora ya mkoani Singida hadi Isaka. Hafla ya utiaji saini wa mkataba huo umefanyika jijini Dodoma na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba kwa upande wa Serikali na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered, Bw. Herman Kasekende.