SERIKALI YANZINDUA PROGRAMU YA USIMAMIZI WA FEDHA ZA UMMA

Serikali imezindua Awamu ya Sita ya Programu ya Maboresho ya Usimamizi wa Fedha za Umma (PFMRP VI) ili kuongeza ufanisi katika kusimamia mapato ya ndani pamoja na kudhibiti matumizi ya fedha za umma. Uzinduzi huo umefanyika jijini Dodoma na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Wizara ya Fedha na Mipango Zanzibar, Mhe. Dkt. Saada Salum Mkuya.