SERIKALI YAKUTANA NA MAKAMPUNI YA SIMU KUJADILI TOZO

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Fedha na Mipango imekutana na Umoja wa Makampuni ya Huduma za Simu Tanzania (TAMNOA) kujadiliana changamoto na faida zilizopatikana kwa watoa huduma hao baada ya utekelezaji wa kukusanya tozo iliyoanzishwa na Serikali.