SERIKALI YAHIMIZA MATUMIZI YA MASHINE YA KIELEKTRONIKI

Serikali ina jukumu kubwa la kuweka mikakati ya kuendelea kurasimisha biashara nchini na kuhamasisha utumiaji wa mashine za kielektroniki katika utoaji wa risiti ikiwa ni pamoja na kutumia risiti hizo kujipatia zawadi kupitia Tuzo ya Uzalendo inayotarajiwa kufunguliwa rasmi hivi punde. Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Kongamano la Kodi, Bw. Robert Manyama, wakati wa Kongamano la Kodi lililofanyika Mkoani Kigoma.