SERIKALI YAANDAA MFUMO WA HUDUMA NDOGO ZA FEDHA

Serikali inaada mfumo wa kielektroniki wa Huduma Ndogo za Fedha ili kuboresha ufanisi wa usimamizi wa Mifuko na Programu za Uwezeshaji wananchi Kiuchumi. Hayo yameelezwa jijini Dodoma na Kamishna Msaidizi wa Idara ya Maendeleo ya Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Dionisia Mjema, wakati akifungua kikaokazi cha kuainisha mahitaji yanayopaswa kuwekwa kwenye mfumo huo.