SERIKALI YAAHIDI KUBORESHA VITUO VYA FORODHA NCHINI

Serikali imeahidi kuboresha vituo vya Forodha mkoani Kilimanjaro, kwa kuweka vifaa vya kisasa, kuboresha majengo ya ofisi hasa jengo upande wa mizigo (Cargo), kuboresha mazingira ya nyumba za watumishi wa kituo hicho na kuongeza vitendea kazi kama vile mdaki. (Scanner kwa upande wa wageni wanaowasili. Amesema hayo Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb), alipotembelea na kufanya ukaguzi kwenye kituo cha forodha kilichopo katika Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Kilimanjaro (KIA) wakati akihitimisha ziara yake ya siku mbili mkoani Kilimanjaro, ambapo amewaahidi kuifanyia kazi changamoto ya vitendea kazi, ikiwemo Midaki (Scanners).