SERIKALI: TUMIENI MIKOPO KUWEKEZA KWENYE BIASHARA ZINAZOZALISHA

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Musoma, mkoani Mara, Bw. Msongela Palela, amewataka wananchi wa Wilaya hiyo kutumia mikopo wanayokopa kufanya uwekezaji unaozalisha faida ili kuepuka kushindwa kufanya marejesho ya mkopo. Bw. Palela alitoa rai hiyo wakati alipokutana na Timu ya Wataalamu kutoka Wizara ya Fedha, Taasisi za Serikali na Binafsi ambayo ipo mkoani Mara kutoa elimu ya fedha kwa makundi mbalimbali.