SERIKALI NA WADAU WA MAENDELEO KUFANYA MKUTANO WA PAMOJA

Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, amefanya kikao na Mwenyekiti Mwenza wa Washirika wa Maendeleo nchini, Mhe. Zlatan Milisic, kuhusu ushirikiano wa maendeleo na maandalizi ya mkutano kati ya Serikali na washirika hao utakaofanyika hivi karibuni. Dkt. Nchemba amefanya kikao hicho jijini Dodoma na Mwenyekiti Mwenza wa Washirika wa Maendeleo nchini, Mhe. Zlatan Milisic, ambapo ajenda mbalimbali za mkutano huo ziliangaziwa.