SERIKALI NA SHIRIKA LA FEDHA LA KIMATAIFA (IMF), ZAHITIMISHA TATHMINI
Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), ameongoza ujumbe wa Tanzania katika kikao cha kuhitimisha tathmini kati ya Serikali na Ujumbe kutoka Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) ulioongozwa na Bw. Charalambos Tsangarides, kwa njia ya mtandao, akiwa jijini Dodoma.
Timu hiyo ya wataalamu kutoka IMF imekuwa nchini kwa majuma kadhaa ikifanya Tathmini ya Awamu ya Nne ya utekelezaji wa Program ya Extended Credit Facility-(ECF), inayohusisha upatikanaji wa mkopo nafuu kwa ajili ya kuimarisha uchumi wa nchi kupitia sekta za uzalishaji na huduma za jamii pamoja na kufanya mapitio na tathmini ya kwanza (1st Review) ya Program mpya ya Serikali ya kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi kupitia Dirisha la Resilient and Sustainable Fund (RSF).