SERIKALI KUTUMIA VIKAO RASMI KUTOA ELIMU YA FEDHA

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Muleba, Bw. Isaya Mbenje, amesema kuwa Serikali itaanza kutumia vikao vyake rasmi kutoa elimu ya huduma ndogo za fedha ili kupunguza migogoro inayoendelea nchini kuhusu mikopo na watu kuchukuliwa mali zao kwa kushindwa kulipa mikopo. Bw. Mbenje alitoa ahadi hiyo wakati alipokutana na Timu ya Wataalamu ya Wizara ya Fedha ambayo ilifika Kisiwa cha Bumbire kutoa elimu ya fedha kwa Wananchi wa Kisiwa hicho ili waweze kujikomboa kiuchumi.