SERIKALI KUPITIA UPYA SERA YA UTALII
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Fedha na Mipango inataka kupitia upya sera za utalii ili kuendana na uhalisia wa mazingira, hayo yamesemwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Lawrence Mafuru alipokuwa akifungua kikao kazi na sekta binafsi chenye lengo la kupata uelewa zaidi kuhusiana na shughuli za utalii kilichofanyika jijini Arusha kwa njia ya mtandao.