SERIKALI KUIMARISHA ZAIDI UWEZESHAJI WA WANAWAKE KIUCHUMI

Serikali imeahidi kuendelea kuimarisha juhudi za uwezeshaji wa wanawake kiuchumi kupitia sekta ya fedha, ikitambua kuwa eneo hilo ni nguzo muhimu katika kukuza uchumi jumuishi na endelevu nchini. Hayo yamesemwa na Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), wakati akifungua Mkutano wa Tatu wa Wanawake katika Sekta ya Fedha (Women in Finance Conference 2026), ulioandaliwa na Chama cha Wanawake katika Sekta ya Fedha Tanzania (Tanzania Women in Finance Association- TAWiFA), katika Jengo la Papu Tower, jijini Arusha.